Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022

SIKU 21 YA 31

Akawapa uwezo na mamlaka juu ya pepo wote na kuponya maradhi (m.1). Sisi watumishi wa kanisa tuna wajibu mbali mbali. Lakini hatuna uwezo au amri ya kiroho ya kutenda kazi yetu asipotupa Bwana Yesu. Sio sisi tuliomchagua yeye. Ndivyo Yesu anatuambia akisema, Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni (Yn 15:16). Hatuwezi kusema kwa mtu: "nakuponya ugonjwa wako", au "pepo nakuamuru toka", au "nakusamehe dhambi zako." Lazima tuongeze neno: "kwa jina la Yesu". Hapo tunaweza kusema kama wanafunzi wa Yesu waliorudi kwa furaha, wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako (10:17). Hatuwezi kujitakia wajibu fulani katika kanisa. Hatuwezi kujipatia wenyewe mamlaka. Ukifanya hivyo si mtumishi wa kweli, maana hali halisi ni kama Paulo anavyotukumbusha katika 1 Kor 12:11, Kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye.

Andiko

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Oktoba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

http://www.somabiblia.or.tz