Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022

SIKU 23 YA 31

Akawaonya, akawakataza wasimwambie mtu neno hilo (m.21). Mbona wasiwatangazie watu kwamba yeye ni Kristo wa Mungu? Ni kwa sababu Wayahudi walikuwa wameshika tu yale maneno ya manabii yanayosema kwamba Kristo atakuwa mtawala wa dunia hii. Lakini unabii unaosema kwamba kwanza itabidi Kristo ateseke na kufa na kufufuka walikuwa hawajautambua (katika m.22 Yesu anasema, Imempasa Mwana wa Adamu kupata mateso mengi, na kukataliwa na wazee na wakuu wa makuhani na waandishi, na kuuawa na siku ya tatu kufufuka). Kwa hiyo aliogopa watu watakuja kwa nguvu kumfanya awe mfalme wao. Hivyo wangepoteza lengo la Mungu kwa maisha yake. Kwa mfano katika Yn 6:14-15 imeandikwa: Basi watu wale, walipoiona ishara aliyoifanya, walisema, Hakika huyu ni nabii yule ajaye ulimwenguni. Kisha Yesu, hali akitambua ya kuwa walitaka kuja kumshika ili wamfanye mfalme, akajitenga, akaenda tena mlimani yeye peke yake.

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Oktoba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

http://www.somabiblia.or.tz