Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022

SIKU 24 YA 31

Waliuona utukufu wake (m.32). Tukio hili ni kutimizwa kwa neno la Yesu katika m.27 anaposema, Nami nawaambia kweli, Wapo katika hawa wanaosimama hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hata wauone kwanza ufalme wa Mungu. Ndugu msomaji, angalia kwa makini sana m.35: Sauti ikatoka katika wingu, ikisema, Huyu ni Mwanangu, mteule wangu, msikieni yeye. Ole wako, usiyeyazingatia maneno haya! Ole wako, unayekataa kumsikia na kumwamini Yesu. Huyu Yesu ambaye Mungu Mwenyezi mwenyewe kwa sauti kutoka mbinguni amemtangaza kuwa ndiye Mwana wake, mteule wake. Zingatia Yesu anavyosema katika m.26, Kila atakayenionea haya mimi na maneno yangu, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo, atakapokuja katika utukufu wake na wa Baba na wa malaika watakatifu. Kumbuka pia ilivyoandikwa katika 2 Pet 1:17-18: Ikiwa mnamwita Baba, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni. Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu. Ndugu nakusihi, umpokee Yesu! Hakuna wokovu katika jina jingine! (Mdo 4:12, Hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo).

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Oktoba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

http://www.somabiblia.or.tz