Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022Mfano

Binti, imani yako imekuponya; enenda zako na amani (m.48). Yesu alitaka huyo mama apate tena kuheshimika na watu. Maana mwanamke mwenye hali yake alihesabiwa kuwa najisi na alitengwa na watu. Kwa hiyo Yesu hakukubali ajifiche, bali uponyaji wake lazima ujulikane kwa wote ili awe tena na maisha mema. Basi, Yesu akamweleza mbele ya watu wote. Kumbuka pia ilivyoandikwa katika Rum 10:10, Kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. Ni imani gani iliyomponya? Ni imani ya kumwamini Yesu. Imani hii ilimfanya alete taabu yake kwa Yesu. Je, utakubali kuacha njia zako za upotovu na kumtegemea Yesu aliye njia ya kweli?
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Oktoba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
http://www.somabiblia.or.tz