Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022Mfano

Nikawasihi wanafunzi wako wamtoe, wasiweze (m.40). Kwa nini hawakuweza? Yesu alishawapa mamlaka juu ya pepo pale alipowaita, akawapa uwezo na mamlaka juu ya pepe wote na kuonya maradhi(9:1). Na walitumia mamlaka hii kwa mafanikio mazuri, maana tunasoma katika 9:6, Wakaenda, wakazunguka katika vijiji, wakihubiri injili, na kupoza watu kila mahali. Lakini siku hiyo walishindwa, kwa nini? Yesu anatoa sababu: walikosa imani (m.41). Tukisoma maelezo ya Injili za Mathayo na Marko twapata kuelewa zaidi. Hapo imeandikwa kwamba Yesu akawaambia, Namna hii haiwezi kutoka kwa neno lo lote, isipokuwa kwa kuomba (Mk 9:29). Yaani walikuwa wametegemea zaidi nguvu yao kuliko kumtegemea Mungu. Kukosa kumtegemea Mungu kwa maombi ni kukosa imani.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Oktoba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
http://www.somabiblia.or.tz