Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Januari 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Januari 2021

SIKU 31 YA 31

Mambo mengi yanawasumbua wana wanaomtumaini Mungu. Mazomeo na dhihaka kutoka kwa watu wasioamini huwalenga ili yamkini waache kumwamini na kumtegemea Mungu. Lakini Mungu huwafanyia nini wote wanaotegemea? Zingatia ulivyosoma katika m.3, Wewe, Bwana, U ngao yangu pande zote, Utukufu wangu na mwinua kichwa changu. Hakika Bwana yu karibu sana na wote wamtumainiao. Huwahakikishia wokovu, malazi salama, usingizi mnono, na kuamka salama. Hata wawapo katikati ya maadui wengi, wamtumainiao Bwana hawana sababu ya kuhofu chochote, maana wokovu una Bwana. Rudia m.6-8, ukiyatumia maneno katika sala yako, Sitayaogopa makumi elfu ya watu, Waliojipanga juu yangu pande zote.Bwana, uinuke, Mungu wangu, uniokoe, Maana umewapiga taya adui zangu wote; Umewavunja meno wasio haki.Wokovu una Bwana; Baraka yako na iwe juu ya watu wako.

Andiko

siku 30

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Januari 2021

Soma Biblia Kila Siku Januari 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Wakorintho. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kuji...

More

Tungependa kushukuru kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha