Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Januari 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Januari 2021

SIKU 24 YA 31

Sehemu hii ya Zab.2 ni utabiri wa utawala na mamlaka juu ya vitu vyote ambayo Mungu amemwahidi Kristo Yesu (m.8, Nitakupa mataifa kuwa urithi wako, na miisho ya dunia kuwa milki yako). Kila amwaminiye afurahie mamlaka yake, maana ahadi ilitimia Yesu alipofufuka (Mt 28:18, Yesu akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani). Leo tunaamini ni kweli; Yesu atakapofunuliwa tutaona kwa macho. Ila kwa wote watakaokaidi, Yesu atafanyika kuwa kikwazo (1 Pet 2:6,8, Imeandikwa katika maandiko: Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima, na kila amwaminiye hatatahayarika. ... Tena, Jiwe la kujikwaza mguu, na mwamba wa kuangusha). Somo latoa wito kwa watu wote watumie busara wakijitiisha kwake, kwani ni hakika: kwake kila goti litapigwa (Flp 2:9-10, Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi). Jisalimishe kwa Kristo Yesu.

siku 23siku 25

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Januari 2021

Soma Biblia Kila Siku Januari 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Wakorintho. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kuji...

More

Tungependa kushukuru kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha