Soma Biblia Kila Siku 03/2025Sample

Wakishika mapokea ya wazee wao(m.3), Wayahudi walidhani wataweza kufikia hali ya kuwa safi mbele ya Mungu. Lakini Yesu anafundisha leo kwamba haiwezekani, maana maovu yanatokandani ya mioyoya watu.Akasema, Kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, ... Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi(m.20-23). Na mioyo haiwezi kusafishwa kwa sheria hizo. Utabaki kuwa usafi wa nje tu. Kwa sababu hiyo Yesu alimfundisha Nikodemo kuwa lazima tuzaliwe upya, tuzaliwe kwa Roho. Bila hivyo hatuwezi kuuingia Ufalme wa Mungu! Inawezekanaje kuzaliwa upya? Zingatia ilivyoandikwa katika Eze 36:25-28 na 1 Yoh 1:17:Nami[Bwana MUNGU]nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote. Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama. Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda.– Tukienenda nuruni, kama[Mungu]alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote!
Scripture
About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 03/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Machi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko, 1 Nyakati na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Related Plans

Love People?!

Sundays at the Track

Move People Through God Alone

Christosis: Participation in Christ and Imitation of Christ

Live Your OWN Life With Conviction

The Family Business: Living Like Jesus. Loving Like Jesus. Leading Like Jesus.

Made for More

Parables of Grace: Embrace God’s Love for You

Anchored: The Life and Letters of the Apostle Peter
