Soma Biblia Kila Siku 11/2024Sample

Mfalme Manase alitumia vibaya sana madaraka yake na kurudisha ibada ya miungu migeni katika Israeli.Akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, sawasawa na machukizo ya mataifa, aliowafukuza Bwana mbele ya wana wa Israeli. Kwa maana akapajenga tena mahali pa juu alipopaharibu Hezekia baba yake; akamjengea Baali madhabahu, akafanya Ashera kama alivyofanya Ahabu mfalme wa Israeli. Akajiinama mbele ya jeshi lote la mbinguni na kulitumikia. Akazijenga madhabahu ndani ya nyumba ya Bwana, napo ndipo alipopanena Bwana, Katika Yerusalemu nitaliweka jina langu. Akajenga madhabahu kwa ajili ya jeshi lote la mbinguni katika behewa mbili za nyumba ya Bwana. Akampitisha mwanawe motoni, akatazama bao, akafanya uganga, akajishughulisha na hao wenye pepo wa utambuzi, na wachawi; akafanya mabaya mengi machoni pa Bwana, hata kumkasirisha. Akaiweka sanamu ya kuchongwa ya Ashera aliyoifanya ndani ya nyumba, ambayo Bwana alimwambia Daudi, na Sulemani mwanawe, Katika nyumba hii, na katika Yerusalemu, niliouchagua miongoni mwa kabila zote za Israeli, nitaliweka jina langu milele(m.2-7). Na vibaya zaidi, aliwakosesha watu wa Mungu wafanye mabaya. Hata hivyo Mungu alimvumilia Manase akimpa utawala wa miaka 55 kabla ya kuamua kuadhibu. Hii itufundishe kwamba tusidharau wingi wa wema wa Mungu. Hata kama sisi wanadamu tungeweza kuendelea kuishi maisha ya dhambi muda mrefu, tujue kuwa Mungu anatuona na kwamba, kama tusipotubu, siku moja ataadhibu maovu na waovu wote.
Scripture
About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 11/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi na moja pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Related Plans

Seasons of Hardship: Live the Jesus Way

UNPACK This...Being a Good Teammate in Life

Am I Really a Christian?

Positive and Encouraging Thoughts for Women: A 5-Day Devotional From K-LOVE

Who Am I, Really? Discovering the You God Had in Mind

Overcoming the Trap of Self-Pity

16 Characteristics of the God-Kind of Love - 1 Corinthians 13:4-8

Don’t Know What You’re Doing After Graduation? Good.

Living Like Jesus in a Broken World
