YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 11/2024Sample

Soma Biblia Kila Siku 11/2024

DAY 28 OF 30

Mfalme wa Babeli alituma wajumbe kuja kumpa pole Mfalme Hezekia kwa kuugua. Katika furaha yake, Hezekia aliwaonyesha wageni utajiri wote katika ufalme wake wote. Hivyo Hezekia alijiamini kupita kiasi, akiweka hadharani yaliyostahili kuwa siri katika ufalme wake. Nabii Isaya alikuja na neno la BWANA juu ya yale aliyofanya mfalme. Mali yote aliyoiweka wazi itachukuliwa, na watoto wake watafanywa kuwa watumishi huko Babeli. Tujihadhari katika kujiamini ili tusijitegemee kuliko kumtegemea Mungu.