Soma Biblia Kila Siku 11/2024Sample

Yesu anatufundisha tabia inayoleta heshima mbele ya Mungu. Ni tabia ya kuwajali sanawadogo hao waniaminio(m.6). Hao ni watoto. Tena ni mtu ye yote aliyekubali kujinyenyekeza na kumpokea Yesu kama Mwokozi wake. Zingatia Yesu anavyoungana na hao akimsema:Kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi. ... Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi(Mt 25:40, 45). Wengi wao si watu wenye vyeo. Kwa hiyo huitwawadogo– au hatawatoto wachanga:Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga.Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako(Mt 11:25-26). Hiyo humfanya Paulo kuwakumbusha Wakristo wa Korintho:ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa;bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu;tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko;mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu.Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi;kusudi, kama ilivyoandikwa, Yeye aonaye fahari na aone fahari juu ya Bwana(1 Kor 1:26-31). Yesu yuko ndani ya wote wanaomwamini, kwa hiyo ukiwapokea wanaomwamini Yesu unampokea mwenyewe. Ukiwadharau unamdharau Yesu. Basi, tuwajalikwanzawalio wa Yesu, na pamoja nao pia wengine wote!
Scripture
About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 11/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi na moja pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Related Plans

God's Book: An Honest Look at the Bible's Toughest Topics

30 Powerful Prayers for Your Child Every Day This School Year

You Say You Believe, but Do You Obey?

Rebuilt Faith

24 Days to Reflect on God's Heart for Redemption

Game Changers: Devotions for Families Who Play Different (Age 8-12)

Awakening Faith: Hope From the Global Church

Protocols, Postures and Power of Thanksgiving

Sharing Your Faith in the Workplace
