YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 08/2024Sample

Soma Biblia Kila Siku 08/2024

DAY 18 OF 31

Kazi ya askofu, yaani mwangalizi wa kanisa, ni njema. Lakini pia ina wajibu na majukumu mengi, tena ni lazima maisha ya askofu yawe kielelezo kwa wote. Hakuna dhambi ndogo. Askofu akikosea kwa namnayoyotesifa zile zilizotajwa katika somo, atakuwa kikwazo kikubwa kwa watu kuingia katika ufalme wa Mungu. Tusikimbilie kuwa watumishi wa Mungu ikiwa hatukubali kuacha ubinafsi na dhambi nyingine. Kanisa linahitaji kutunzwa. Ni vivyo hivyo na askofu mwenyewe. Kwa hiyo yapo masharti yafuatayo:Asiwe mtu aliyeongoka karibu, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi. Tena imempasa kushuhudiwa mema na watu walio nje; ili asianguke katika lawama na mtego wa Ibilisi(m.6-7).

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 08/2024

Soma Biblia Kila Siku 08/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Nane pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 2 Wafalme na 1 Timotheo. Karibu kujiunga na mpango huu

More