YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 08/2024Sample

Soma Biblia Kila Siku 08/2024

DAY 20 OF 31

Je, unajuasiri ya utauwani nini? Hatuwezi kusema hatujui, kwa sababu Mungu ametujulisha. Amejifunua katika Yesu Kristo. Alikuja kwetu kimwili katika Mwana wa Mungu, kama ilivyoelezwa wazi katika Yn 1:1, 14 na 18:Neno alikuwa Mungu ... Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu … Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua. Yesu Kristo ndiye habari njema ya wokovu wetu. Amekwenda kutuandalia makao ya milele pale alipo yeye sasa katika utukufu wa mbinguni, kama tunavyokumbushwa katika m.16:Mungu alidhihirishwa katika mwili, ... Akachukuliwa juu katika utukufu. Tukijua siri hiyo, itatufahamisha mwenendo wa kikristo,[t]upate kujua jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu, iliyo kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msingi wa kweli(m.15). Tena itatusukuma kuwajulisha na wengine wote duniani kote ujumbe huu wa Kristo ili na wao waokolewe naye.

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 08/2024

Soma Biblia Kila Siku 08/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Nane pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 2 Wafalme na 1 Timotheo. Karibu kujiunga na mpango huu

More