YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 06/2024Sample

Soma Biblia Kila Siku 06/2024

DAY 11 OF 30

Kila mwanadamu amewekewa mwisho wa kufanya kazi hapa duniani. Hata kazi iwe nzuri namna gani mwisho ni lazima. Paulo anaona sasa mwisho wa kazi yake duniani umekaribia. Amefanya kazi kwa bidii na dhamiri yake inamshuhudia vema.Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda(m.7). Je, inawezekana haya maneno kuwa yako ufikiapo mwisho wa kazi yako hapa duniani? Jihoji. Na tuhimizane kutolegea katika imani, bali kufanya bidii ya kueneza Injili mahali popote tulipo.

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 06/2024

Soma Biblia Kila Siku 06/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa sita pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 2 Timotheo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu

More