Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022Sample

Yesu hakunawa kabla ya chakula (m.38). Wayahudi walikuwa na desturi ya kunawa kabla ya chakula ili wawe safi kidini. Kusudi la Yesu kutonawa ni kupata nafasi ya kuwasema Mafarisayo na Waandishi (‘wana-sheria’). Maana usafi wao ulikuwa wa nje tu. Hawakutubu moyoni. Tafakari Yesu anavyoeleza hali yao: Ndani yenu mmejaa unyang’anyi na uovu ... mwaacha mambo ya adili, na upendo wa Mungu ... mwawatwika watu mizigo isiyochukulika, wala ninyi wenyewe hamwigusi mizigo hiyo hata kwa kimoja cha vidole vyenu (m.39, 42, 46). Kwa hiyo Yesu anawaambia, Toeni sadaka vile vya ndani, na tazama, vyote huwa safi kwenu (m.41). Jambo kuu kwa Mungu ni haki (‘adili’) na upendo (m.42). Je, umetubu moyoni na kuyazingatia yale yaliyo muhimu machoni pa Mungu? Au Ukristo wako ni wa nje tu? Zingatia ilivyoandikwa katika Isa 1:15-18: Nanyi mkunjuapo mikono yenu, nitaficha macho yangu nisiwaone; naam, mwombapo maombi mengi, sitasikia; mikono yenu imejaa damu. Jiosheni, jitakaseni; ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu; acheni kutenda mabaya; jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane. Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.
Scripture
About this Plan

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Disemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Related Plans

FruitFULL - Faithfulness, Gentleness, and Self-Control - the Mature Expression of Faith

Peace in Chaos for Families: 3 Days to Resilient Faith

Daniel in the Lions’ Den – 3-Day Devotional for Families

The Bible, Simplified

Spring of Renewal

Connect

Rich Dad, Poor Son

What Is My Calling?

Beautifully Blended | Devotions for Couples
