Soma Biblia Kila Siku Julai/2022Sample

Mariamu alipokea ujumbe wa malaika kwa unyenyekevu na utii: Iwe kwangu kama ulivyosema (m.38). Katika hili ni mfano kwetu namna ya kuliheshimu na kulitii Neno la Mungu katika maisha yetu, hata likituambia jambo lipitalo uwezo wetu wa kuelewa. Somo la leo linatueleza jinsi Mariamu alivyobarikiwa na Mungu baada ya kufanya uamuzi wa kuukubali ujumbe wake. Elisabeti akasema, Umebarikiwa wewe katika wanawake, naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa (m.42). Na Mariamu mwenyewe anasema, Tokea sasa Vizazi vyote wataniita mbarikiwa (m.48). Ni binti aliyelitafakari sana Neno la Mungu, maana katika kumsifu Mungu hutumia maneno mengi kutoka A/K. Linganisha m.54-55 inayoeleza kuwa Mungu amemsaidia Israeli, mtumishi wake; Ili kukumbuka rehema zake; Kama alivyowaambia baba zetu, Ibrahimu na uzao wake hata milele, na Mwa 22:15-18, Malaika wa Bwana akamwita Ibrahimu mara ya pili kutoka mbinguni akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema Bwana, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee, katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao; na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu.
Scripture
About this Plan

Soma Biblia Kila Siku Julai/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Julai pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Zakaria na Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Related Plans

Game Changers: Devotions for Families Who Play Different (Age 8-12)

Legacy Lessons W/Vance K. Jackson

Awakening Faith: Hope From the Global Church

Protocols, Postures and Power of Thanksgiving

Rebuilt Faith

God's Book: An Honest Look at the Bible's Toughest Topics

30 Powerful Prayers for Your Child Every Day This School Year

24 Days to Reflect on God's Heart for Redemption

You Say You Believe, but Do You Obey?
