YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku Juni/2022Sample

Soma Biblia Kila Siku Juni/2022

DAY 5 OF 30

Mungu ana nguvu isiyo ya kawaida, na ahadi zake ni za kweli. Kwa njia ya Yesu alitimiza ahadi ya kutuletea Roho Mtakatifu, ambaye ana nguvu, ni mwalimu, tena ni mfariji na mwelekezi. Kutompokea ni sawa na kuwa nje ya matendo makuu ya wokovu wa Mungu. Utii wa imani ya Mitume kwa Yesu ulifanya wampokee Roho Mtakatifu. Ni njia tuliyo nayo sisi pia. Roho Mtakatifu anaingia moyoni mwetu tukimwamini Yesu, na ataendelea kutuongoza tukijinyenyekeza tu kwake na kuwa watii kwa uongozi wake.

Scripture

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku Juni/2022

Soma Biblia Kila Siku Juni/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Juni pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Wafilipi na Mwanzo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More