YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022Sample

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022

DAY 30 OF 31

Huko nyuma tumesoma jinsi Isaka na Yakobo walivyooa kwa heshima na utaratibu mzuri. Tena hawakuoa watu wasiomjua Mungu. Ndivyo inavyotakiwa kwa mtu wa Mungu.  ... mwepukane na uasherati; kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima; si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu (1 The 4:3-5). Kwa hiyo Shekemu alivyomtendea Dina ni jambo baya sana machoni pa Yakobo na wana wake. Akalala naye, akambikiri (m.2), tafsiri yake halisi ni "akalala naye kwa nguvu," yaani, alimbaka! Kwa hiyo wakawa na uchungu sana, maana iliyofanyika ni neno lisilojuzu kutendeka (m.7), yaani, lilikuwa mwiko! Je, wewe umetii amri?

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mwanzo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.

More