YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 06/2020Sample

Soma Biblia Kila Siku 06/2020

DAY 12 OF 30

Somo ni ushuhuda wa Mungu (wa Utatu) kuhusu Mwana wa Mungu. Huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe (m.11). Hakuna wokovu katika jina jingine (= mtu mwingine) ila katika jina la Yesu tu. Yeye ndiye uhai wa kweli – kama anavyosema mwenyewe katika Yn 14:6,Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. Kinyume chake, kuna asiyemwamini Mungu, huyuamemfanya [Mungu]kuwa mwongo (m.10). Sababu ya msingi ya kupotea ni “kutomwamini Mungu”. Je, unaye Mwana katika maisha yako? Amwaminiye Mwana wa Mungu, ushuhuda wake hukaa ndani yake, kwa kuwa Yesu hukaa ndani yake. Yesu yupo ambapo Neno lake lipo na kuaminiwa.

Scripture

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 06/2020

Soma Biblia Kila Siku 06/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Yohana, Ayubu na Mathayo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More