YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 06/2020Sample

Soma Biblia Kila Siku 06/2020

DAY 14 OF 30

Mtu akimwona ndugu yake anatenda dhambi isiyo ya mauti, ataomba (m.16). Mtume hakutofautisha ni dhambi zipi! Je, tunafanya nini tukimwona ndugu yetu akitenda dhambi? Je, tunamcheka? Hapa tunafundishwa kwamba inapotokea yatupasa kuomba. Kuna ahadi njema kwa maombi haya: Mungu atampa uzima. Dhambi iliyo ya mauti (m.16). Maana yake ni nini? Ni dhambi ya kumdharau Mungu na kuudharau wokovu aliotufanyia Yesu. Ni dhambi anayotenda mtu anapouharibu ule uhai aliopewa tayari na Mungu (linganisha na Yesu anavyoeleza Mt 12:32, Mtu ye yote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao). Inawezekana kuwa Yohana anapoandika kuhusu dhambi iliyo ya mauti, anafikiri juu ya hao waliotambulishwa katika barua hii kama wapinga Kristo (k.m. katika 2:22:Ni nani aliye mwongo ila yeye akanaye ya kuwa Yesu ni Kristo? Huyo ndiye mpinga Kristo).