YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 06/2020Sample

Soma Biblia Kila Siku 06/2020

DAY 13 OF 30

Nimewaandikia ninyi mambo hayo (m.13). Yohana akiandika “mambo hayo”, anamaanisha barua nzima. Anataka kutuonyesha kitu. Haandiki “labda” au “kama ukifanya hivi”, bali “mjue”. Kuna uhakika. Si mioyoni mwetu au kwa kujisikia kwetu, bali uhakika wetu wa wokovu hupatikana nje yetu. Tunaupokea kutoka kwa Yesu Kristo.Hilo tuliloliona na kulisikia, twawahubiri na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi; na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo(1:3). Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele(Yn 3:36). Hayo huleta ujasiri na uhuru wa kuomba sawasawa na mapenzi ya Mungu. Hutokana na kuomba katika jina la Yesu. Mwenyewe ameahidi, Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya (Yn14:14). Haya yanaonyesha ushirikiano na uhuru wa pekee uliopo kati ya Kristo na waumini.

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 06/2020

Soma Biblia Kila Siku 06/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Yohana, Ayubu na Mathayo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More