YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 06/2020Sample

Soma Biblia Kila Siku 06/2020

DAY 10 OF 30

Sisi twapenda kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza (m.19). Msingi wa upendo unarudiwa tena. Mungu ni mwanzo, pia mwanzo wa upendo. Wengine wanafikiri kwamba ni rahisi kumpenda mtu wa mbali na mtu ambaye hatujakutana naye bado. Lakini hayo siyo kumpenda mwingine, bali ni kujidanganya. Kama kweli tunao upendo, huo huonekana tunapokutana na ndugu. Zingatia m.21:Amri hii tumepewa na yeye, ya kwamba yeye ampendaye Mungu, ampende na ndugu yake. Upendo wa kweli hatuwezi kuuficha.

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 06/2020

Soma Biblia Kila Siku 06/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Yohana, Ayubu na Mathayo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More