Soma Biblia Kila Siku 10Sample

Yule Mfilisti Goliathi alikuwa ni jitu kweli! Urefu wake ulikuwa karibu mita tatu, na alikuwa amevaa darii ya shaba yenye uzito sawa na madebe matatu ya mahindi! "Darii" ni sawa na "deraya", ambayo ni nguo za vita zilizotengenezwa kwa chuma au shaba. Kichwa au chembe cha mkuki wake kilikuwa na uzito wa kilo saba, na mpini wake ulikuwa na ukubwa sawa na mchi mrefu! Kila siku kwa siku 40 Goliathi alikuja bondeni akiwatukana Waisraeli. Na Waisraeli hawakuwa na mtu wa kumweza, wakaogopa sana. Inaonekana walisahau kabisa uweza wa Mungu!
Scripture
About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 10 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kitabu cha Warumi na 1 Samweli.
More









