YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 10Sample

Soma Biblia Kila Siku 10

DAY 8 OF 31

Basi, Roho wa Bwana ilikuwa imemwacha Sauli, na roho mbaya kutoka kwa Bwana ikamsumbua(m.14). Maana yake nini? Angalia, neno halisemi kwamba Roho wa Bwana ni mbaya! Mungu ni nuru, wala giza lolote hamna ndani yake(1 Yoh 1:5). Basi tutaelewa vipi maneno haya: roho mbaya kutoka kwa Bwana ikamsumbua? Maana yake ni kwamba Bwana ni Mungu Mkuu. Mtu akiwa karibu na Mungu, nguvu za giza haziwezi kumdhuru. Lakini mtu akiachana na Mungu na ulinzi wake, Shetani hupata nafasi ya kumtesa akiruhusiwa na Mungu!