YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 10Sample

Soma Biblia Kila Siku 10

DAY 14 OF 31

Naye Sauli akamwoza Mikali, binti yake. Sauli akaona na kutambua ya kwamba Bwana alikuwa pamoja na Daudi; na huyo Mikali, binti Sauli, akampenda. Naye Sauli akazidi kumwogopa Daudi; Sauli akawa adui yake Daudi siku zote (m.27-29). Ilikuwa ni ahadi ya mfalme kwamba mtu yule atakayemwua Goliathi atapewa binti wa mfalme kama mke wake. Ila binti wa kwanza wa mfalme alishaolewa na mtu mwingine:Ikawa, wakati ule, ilipopasa Daudi apewe Merabu, binti Sauli, aliolewa na Adrieli, Mmeholathi (m.19). Hii ilikuwa ni bahati yake Daudi, maana binti wa pili wa mfalme, Mikali, ndiye aliyempenda (m.20)! Upendo wake huu alionyesha wazi kwa vitendo wakati Sauli, baba yake, alipotaka kumwua Daudi: Kisha Sauli akatuma wajumbe mpaka nyumbani kwa Daudi, ili wamvizie na kumwua asubuhi; naye Mikali, mkewe Daudi, akamwambia, akasema, Wewe usipojiponya nafsi yako usiku huu, kesho utauawa. Basi Mikali akamtelemsha Daudi dirishani; naye akaenda akakimbia na kuokoka(19:11-12).