Soma Biblia Kila Siku 10Sample

Ndipo Daudi akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia mimi na upanga, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la Bwana wa majeshi... watu wote pia wajue ya kwamba Bwana haokoi kwa upanga wala kwa mkuki; maana vita ni vya Bwana, naye atawatia ninyi mikononi mwetu(m.45 na 47). Daudi alivyomshinda adui ni mfano mzuri kwetu Wakristo jinsi ya kupata ushindi katika vita vya kiroho! Mbele ya Goliathi, Daudi si kitu. Pia sisi si kitu mbele ya Shetani, hata tukiwa maprofesa au wanajeshi, ila kwa jina la Yesu Kristo twashinda!Zingatia iliyoandikwa katika 1 Kor 1:26-29: Ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa; bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu; tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko; mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu.
Scripture
About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 10 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kitabu cha Warumi na 1 Samweli.
More









