Soma Biblia Kila Siku 10Sample

Daudi alimwambia Sauli,Mtumishi wako alimwua simba na dubu pia; na huyu Mfilisti asiyetahiriwa atakuwa kama mmoja wao, kwa sababu amewatukana majeshi ya Mungu aliye hai. Daudi akasema, Bwanaaliyeniokoa na makucha ya simba, na makucha ya dubu, ataniokoa na mkono wa Mfilisti huyu(m.36-37). Kijana Daudi alionekana ni shujaa, si kwa uweza wa kibinadamu ila ni shujaa katika kumwamini Bwana na kumtegemea hata hapo ambapo nguvu yake mwenyewe haitoshi. Waisraeli walipotukanwa, ni Mungu mwenyewe aliyetukanwa, maana hao ni watu wake. Hiyo Daudi hawezi kukubali, maana anampenda Bwana!
Scripture
About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 10 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kitabu cha Warumi na 1 Samweli.
More









