YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 10Sample

Soma Biblia Kila Siku 10

DAY 24 OF 31

Sasa Mtume Paulo anaanza kueleza jinsi hali yake ilivyokuwa baada ya kuokoka na kumpata Roho Mtakatifu. Kimsingi maisha yake yamebadilika. Amepata nafsi mpya inayoipenda sheria ya Mungu (torati) na kuyachukia yaliyo kinyume cha mapenzi ya Mungu: Kwa maana naifurahia sheria ya Mungu kwa utu wa ndani(m.22). Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili;ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho(8:3-4). Hata hivyo bado kuna mapambano katika maisha ya Mkristo, Paulo anashuhudia. Dhambi imefaulu kumshinda tena na tena: Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu (m.20). Umeyaona haya maishani mwako?