YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 10Sample

Soma Biblia Kila Siku 10

DAY 28 OF 31

Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho (m.5). Hii ina maana ya kwamba ukitaka kuishinda dhambi katika maisha yako ya Kikristo kwa nguvu zako mwenyewe (waufuatao mwili), utakwama, na utabaki tu kutamani dhambi (huyafikiria mambo ya mwili). Lakiniukimtegemea Kristo na kuufikiria ukombozi aliokushindia (waifuatao roho), maisha yako yatakuwa na matunda mema (huyafikiri mambo ya roho). Zingatia kwa makini Yesu anayosema: Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote(Yn 15:5). Matunda hayo tunayozaa tunapokaa ndani ya Yesu, ni kazi ya Roho anayekaa ndani yetu. Kwa hiyo huitwa tuna la Roho: Tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria(Gal 5:22-23).

Scripture