Soma Biblia Kila Siku 10Sample

Mtume Paulo ameshuhudia jinsi alivyoshindwa kuishi maisha matakatifu baada ya kuwa Mkristo (7:14-25). Ni kwa sababu alipambana kwa nguvu zake mwenyewe. Ingawa alikwisha zaliwa mara ya pili ikaonekana kana kwamba maisha ya dhambi ina nguvu kuliko Roho Mtakatifu. Alikwama na akagundua kosa lake kwamba anatakiwa amtegemee Yesu Kristo badala ya kujitegemea.Ole wangu, maskini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti? Namshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Basi, kama ni hivyo, mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu, bali kwa mwili wangu sheria ya dhambi(7:24-25). Katika somo la leo Paulo anaeleza kwa nini amefurahi namna hiyo. Ni kwa sababu ameona na kutegemea kwamba hayo aliyoshindwa kuyafanya yeye mwenyewe kwa kutegemea msaada wa sheria, hayo Munguameyafanya kwa kumtuma Yesu. Kwa sababu ya ukombozi wa Yesu, Paulo amewekwa huru, maana adhabu imeondolewa, na Roho amepata kumtawala. Hivyo maagizo ya sheria ya Mungu yanaendelea kutimizwa ndani ya Paulo na wengine wote wanaomwamini Yesu Kristo (8:1-4)!
Scripture
About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 10 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kitabu cha Warumi na 1 Samweli.
More
Related Plans

Finding Joy

Elijah: A Man Surrendered to God

And He Dwelt

The Layoff Test: Trusting God Through a Season of Unemployment

The Power of Biblical Meditation

Joyfully Expecting!

Between the Altar and the Father’s Embrace

Mom in the Word: One-Year Bible Plan (Volume 1)

God’s Word, Her Mission: Encouragement for Women Helping Build God’s Kingdom by Wycliffe Bible Translators
