YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 10Sample

Soma Biblia Kila Siku 10

DAY 23 OF 31

Kitu chema, yaani amri za Mungu, kinamfanya mtu kuwa mbaya zaidi! Inakuwaje? Ni kwa sababu tumeirithi dhambi kutoka kwa Adamu (5:19: Kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi). Ndani ya mioyo yetu kuna uadui na Mungu,kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii(8:7). Huu uadui huamka na kujionyesha kwa wazi tunaposikia amri za Mungu na kuamua kuzifuata (m.8-11: Dhambi ilipata nafasi kwa ile amri, ikafanya ndani yangu kila namna ya kutamani. … Ilipokuja ile amri, dhambi ilihuika, nami nikafa. Nikaona ile amri iletayo uzima ya kuwa kwangu mimi ilileta mauti. Kwa maana dhambi, kwa kupata nafasi kwa ile amri, ilinidanganya, na kwa hiyo ikaniua). Ni kama unapotaka kumpa mtu fulani kitu chema, lakini umeshindwa, maana ana mbwa, na unapokaribia nyumba huanza kubweka kana kwamba husema, Hapa natawala mimi, usikaribie! Hivyo sheria hutufanya tuone tumepotea na kuhitaji wokovu! Kama ilivyoandikwa katika Rum 3:19-20:Mambo yote inenayo torati huyanena kwa hao walio chini ya torati, ili kila kinywa kifumbwe, na ulimwengu wote uwe chini ya hukumu ya Mungu; kwa sababu hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria; kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria.

Scripture