YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 10Sample

Soma Biblia Kila Siku 10

DAY 16 OF 31

Sauli alizidi kumchukia Daudi na kutafuta kila njia ili kumwua, ingawa alikuwa ameapa kwa Yonathani akisema: Aishivyo Bwana, yeye hatauawa (m.6). Hali hiyo ilisababishwa na wivu wake pamoja na mapepo mabaya ya Shetani ambayo Mungu aliruhusu yamsumbue Sauli kwa sababu alimwasi (ona maelezo kwa 1 Sam 16:14-23; somo la 8 katika mfululizo huu). Daudi alilindwa na nguvu ya Mungu akiwa Nayothi pamoja na Samweli na  manabii. Habari katika m.20 kuhusu wajumbe aliowatuma Sauli ili wamkamate Daudi, kwamba wakatabiri, ina maana kwamba Roho wa Mungu alikuwa juu yao na kuongoza ulimi wao. Ilipotokea kwa Sauli akachanganyikiwa maana ni mwasi: Sauli akaenda Nayothi huko Rama, na Roho wa Mungu akamjilia yeye naye, akaendelea mbele, huku anatabiri, mpaka kufika Nayothi huko Rama.Naye akavua nguo zake, akatabiri mbele ya Samweli, akalala uchi mchana kutwa na usiku kucha siku ile(m.23-24).

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 10

Soma Biblia Kila Siku 10 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kitabu cha Warumi na 1 Samweli.

More