YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 10Sample

Soma Biblia Kila Siku 10

DAY 18 OF 31

Yonathani akamjibu Sauli, baba yake, akamwambia, Auawe kwa sababu gani? Amefanya nini? Sauli akamtupia mkuki wake ili kumpiga(m.32-33). Chuki ya Sauli haikuwa na sababu ya msingi. Na Daudi na Yonathani  walistaajabu:Daudi … akaenda kwa Yonathani, akasema mbele yake, Nimefanya nini? Uovu wangu ni nini? Dhambi yangu mbele ya baba yako ni nini, hata akaitaka roho yangu?  (20:1). Pia hutokea kwamba sisi Wakristo tunaudhiwa na mtu bila sababu ya msingi. Yesu alitueleza sababu: Wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu. Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa (Yn 3:19-20). Pia anasema katika Yn15:18-21: Iwapo ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi. Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia. Likumbukeni lile neno nililowaambia, Mtumwa si mkubwa kuliko bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi; ikiwa walilishika neno langu watalishika na lenu. Lakini haya yote watawatenda kwa ajili ya jina langu, kwa kuwa hawamjui yeye aliyenipeleka.