Soma Biblia Kila Siku 10Sample

Hapa tunafundishwa jambo moja muhimu linalotusaidia kupata ushindikatika maisha yetu ya Kikristo! Katika Yesu Kristo tunahesabiwa kuwa wenye haki mbele ya Mungu. Lakini kuna zaidi ya hayo, maana hata nguvuya dhambi tumekombolewa nayo katika Yesu Kristo (m.6: Utu wetu wa kale ulisulibishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena)! Kwa njia ya ubatizo na imani tumeunganika na Yesu (m.3-5: Sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima. Kwa maana kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake). Kwa hiyo tunashiriki katika ushindi wake Yesu. Yaliyotendeka kwake pia yametendeka kwetu! Ndivyo ilivyoandikwa hapa katika m.8-11. Dhambi ikitaka kukutawala tena, shika maneno haya nawe utashinda. Fikiria zaidi ushindi wa Yesu una matokeo gani kwako unayemwamini: Kwa kule kufa kwake, aliifia dhambi mara moja tu; lakini kwa kule kuishi kwake, amwishia Mungu. Vivyo hivyo ninyi nanyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi na walio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu(m.10-11).
Scripture
About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 10 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kitabu cha Warumi na 1 Samweli.
More
Related Plans

Finding Joy

Elijah: A Man Surrendered to God

And He Dwelt

The Layoff Test: Trusting God Through a Season of Unemployment

The Power of Biblical Meditation

Joyfully Expecting!

Between the Altar and the Father’s Embrace

Mom in the Word: One-Year Bible Plan (Volume 1)

God’s Word, Her Mission: Encouragement for Women Helping Build God’s Kingdom by Wycliffe Bible Translators
