YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 10Sample

Soma Biblia Kila Siku 10

DAY 15 OF 31

Yonathani alifanya kazi nzuri ya upatanishaji kati ya baba yake Mfalme na rafiki yake Daudi! Alimhakikishia Sauli kwamba hakuna sababu ya kumchukia Daudi. Ndipo Daudi akarudi kukaa karibu na mfalme. Katika hili Yonathani ni mfano mzuri kwetu Wakristo. Yesu ametuambia: Heri wapatanishi; maana hao wataitwa wana wa Mungu (Mt 5:9). Mkristo wa kweli hapendi ugomvi, bali hutafuta amani. Anajitahidi kuwa mpatanishi kati ya watu kwa maneno na kwa matendo. Maana ana roho ya Mungu, Baba yake, ndani yake! Jinsi hiyo inavyoonekana katika maisha yake, unaweza kusoma katika Rum 12:14-21.