YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 6Sample

Soma Biblia Kila Siku 6

DAY 23 OF 30

Sauti ya Mungu hutuita katika hali mbalimbali. Inatuita hata sasa kwa njia ya neno hili la leo. Lengo la Mungu ni kutushauri tuache ujinga, upumbavu na dharau. Kutoisikiliza sauti ya Mungu ndiko kunakosababisha kukosa utii kwake. Matokeo ya kutotii ni kutengwa na Mungu. Tunapohitaji msaada kwake hatatusikiliza. Hakuna kitu kichungu kuliko kuachwa na Mungu. Ukikosa Mungu, utapata wapi kimbilio? Mtii Mungu, na utakuwa na amani na mafanikio. Rudia m.23 ukizingatia maana yake katika maisha yako: Geukeni kwa ajili ya maonyo yangu; Tazama, nitawamwagia roho yangu, Na kuwajulisheni maneno yangu.