YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 6Sample

Soma Biblia Kila Siku 6

DAY 22 OF 30

Ila watu hao wamekwisha kutangulia wakatungojea Troa (m.5). Hapa tunaona kwamba Luka aliye mwandishi wa kitabu hiki mwenyewe alikuwa pamoja na Paulo katika safari hii (wakatungojea). Yaani ni shahidi wa mambo haya. Jambo hili pia tunaona katika safari yake ya pili (16:10-16). Luka alikuwa mtu aliyekuwa karibu sana na Paulo kwa hiyo alijua vizuri sana habari za safari zake (2 Tim 4:11; Flm 24). Tena ni mtu mwenye elimu (daktari; Kol 4:14). Uyunani(m.2) ni upande wa kusini mwa Makedonia (k.m. sehemu za Athene na Korintho).

Scripture