YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 6Sample

Soma Biblia Kila Siku 6

DAY 25 OF 30

Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe (m.28). Mtumishi wa Bwana hapa ajifunze: 1.Asifikirie kulitunza kundi tu lakini pia akumbuke kujitunza nafsi yake! 2.Kwa njia gani atunze kundi na nafsi yake? a) Alishe kwa neno la neema (m.28: Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe; m.32: Nawaweka katika mikono ya Mungu, na kwa neno la neema yake, ambalo laweza kuwajenga na kuwapa urithi pamoja nao wote waliotakaswa). b) Alinde(m.29-30 inatoa sababu: Mbwa-mwitu wakali wataingia kwenu, wasilihurumie kundi;tena katika ninyi wenyewe watainuka watu wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao). c) Akeshe(m.31:kesheni, mkikumbuka ya kwamba miaka mitatu, usiku na mchana). d) Aonye(m.31: Sikuacha kumwonya kila mtu kwa machozi). e) Ajiweke mikononi mwa Mungu(m.32: Nawaweka katika mikono ya Mungu). f) Awasaidie wanyonge (m.35: Kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge). 3.Kanisa si lake Paulo (wala mtu mwingine yeyote), bali ni mali ya Yesu!

Scripture