Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 07/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 07/2025

SIKU 22 YA 31

Ukristo wetu unatakiwa uonekane hasa siku za shida na taabu. Hapo ndipo itaonekana hasa kuwa kuna roho gani ndani yako na kimbilio lako ni nani!Maana huu ndio wema hasa, mtu akivumilia huzuni kwa kumkumbuka Mungu, pale ateswapo isivyo haki(m.19). Kuwa na roho ya jinsi hiyo ni kuwa na Roho wa Kristo ndani yetu, maana ndivyo alivyokuwa Yesu.Alipoteswa, hakuogofya; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki(m.23). Kwa kuzingatia mfano huo wa Yesu, Paulo anatuhimiza:Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote. Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote. Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana. Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake. Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema(Rum 12:17-21). Je, umekuwa na tabia gani mbele ya mwajiri wako?

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 07/2025

Soma Biblia Kila Siku 07/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Julai pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Isaya na 1 Petro. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz

Mipangilio yanayo husiana