Mbazi za YesuMfano

KONDOO MPOTEVU NA SARAFU ILIYOPOTEA
Mbazi hizi mbili zililengwa kwa Wafarisayo na waandishi walipolalamika kuhusu jinsi Yesu aliwajali "wenye dhambi na watoza ushuru."
Upendo wa Yesu kwa wapotevu ulikuwa tofauti sana na hukumu ya viongozi wa kidini wa siku hiyo. Yesu anawaambia namna ambavyo mbinguni ni kama mtazamo wake, wala si mtazamo wa hukumu wa Wafarisayo, anawaeleza kwamba mbingu inashangilia mtu mmoja mwenye dhambi akitubu.
Tunapozidi kumfuata Mungu, inakuwa rahisi kufikiri kwamba tu wema kama Wafarisayo, kwa hivyo tunafaa kujiuliza kuwa tunafanyaje tunapoona hata mtu mmoja mwenye dhambi akitubu. Tunafaa kujiuliza ni nini tunafanya ili kuwatafuta "kondoo wapotevu" na "sarafu zilizopotea" karibu nasi. Ni muhimu tuwe na shauku ya "watu hao," na kufanya kila kitu tuwezayo kuwasaidia kumpata Yesu, na kushangilia kwa sauti nao wanapotubu.

Andiko
Kuhusu Mpango huu

Mpango huu utakuwezesha kusoma mbazi za Yesu na kuchunguza maana ya mafunzo yake kwako! Unaweza kuendelea na mpango wako ulipoachia kwani imerahisishwa kufika ulipokuwa. Hii itakupa wakati kutafakari na kuhamasishwa na upendo na nguvu wa Yesu!
More
We would like to thank Trinity New Life Church for this plan. For more information, please visit: http://www.trinitynewlife.com/