Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023

SIKU 23 YA 30

Kuijua haki, kuitenda na kuifuata ni jambo la watu wote. Wakristo wanaitwa kuongoza wengine katika kutekeleza hili. Wakristo waishipo kwa haki, maisha yao yanakuwa ushuhuda wa Kristo. Je, Mungu anatawala na kuongoza mafanikio yako? Je, wewe hapo ulipo kazini na nyumbani, unaishi na kutenda haki ya Mungu? Kama hutendi haki, basi, unawaonea watu wa Mungu na Mungu mwenyewe.Kama ningaliwaza maovu moyoni mwangu, Bwana asingesikia(Zab 66:18).Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako; ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu. Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimuLk 13:25-27). Jiulize mali ulizo nazo zinatokana na mapato halali? Zingatia m.6:Afadhali maskini aendaye katika unyofu wake, kuliko mpotofu wa njia ingawa ni tajiri!

siku 22siku 24

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa septemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi k...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha