Maelezo ya mpango
Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023Mfano
![Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F39420%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Ni baraka na fanaka kunapokuwapo watu wanaoujua wema na haki miongoni mwa jamii. Hawa huwa viongozi waongozao bila dhuluma, ubadhirifu, ubinafsi, chuki wala kisasi. Waovu wanapotawala huleta vurugu na kutoweka kwa amani kwa wote. Waijuao haki huongoza na kutoa hukumu kwa huruma (1 Tim 5:20,Wale wadumuo kutenda dhambi uwakemee mbele ya wote, ili na wengine waogope). Ombea taifa lako ili Mungu alioneshe viongozi wanaoijua haki na kuishi kwayo. Mtafute Bwana ili uwe na haki hiyo wewe mwenyewe. Itakuwezesha kupigana na uovu.Wao waiachao sheria huwasifu waovu; bali wao waishikao hushindana nao. Watu wabaya hawaelewi na hukumu; bali wamtafutao Bwana huelewa na yote(m.4-5).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
![Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F39420%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa septemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi k...
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/