Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023

SIKU 25 YA 30

Ujumbe huu ni endelezo la neno latika 28:19,Alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele; bali afuataye mambo ya upuzi atapata umaskini wa kumtosha. Mungu anapenda watu wote wafanikiwe maishani kwa njia za halali. Usiwasifie wapatao mali kwa hila na dhuluma, bali uwasaidie watubu. Bila kumtegemea Mungu mafanikio yote hushindwa na hupotea haraka. Tukimtegemea Mungu tutapata cha kututosha. Naam, hatutatindikiwa hata kitu kwa ajili ya kuwakarimu wanyonge na maskini wanaotuzunguka hapo tulipo.Mwenye kuwagawia maskini hatahitaji kitu; bali afichaye macho yake atakuwa na laana nyingi(m.27).Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema(2 Kor 9:8).

siku 24siku 26

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa septemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Warumi na Methali. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/