Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023

SIKU 26 YA 30

Jamii inahabarishwa umuhimu wa kuwa na viongozi na watu wanaoijua na kuitenda haki. Usikaidi unapoonywa, maana tokeo lake ni baya. Lakini waijuao haki hupata maarifa ya kutambua na kuijutia dhambi na uovu wao.Mtu akighafilika katika kosa lo lote, ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe(Gal 6:1). Hakuna jamii ipendayo ubaya, maana haki ikipuuzwa, familia na taifa huangamia. Hata waovu hawapendi watoto wao waige uovu wao. Mungu anaagiza haki itendeke. Haki ni tabia ya Mungu. Penda haki na uitende, ndivyo Mungu anavyotaka kwako.Ee mwanadamu, yeye amekuonyesha yaliyo mema; na Bwana anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenye kwa unyenyekevu na Mungu wako(Mik 6:8)!

siku 25siku 27

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa septemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi k...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha