Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mtazamo Wa Kibiblia Kuhusu Mabadiliko Katika JamiiMfano

A Biblical View On Social Change

SIKU 5 YA 5

Ushindi

Yesu haridhiki watu wakibaki wahitaji. Tunaona haya katika somo kutoka Injili ya Marko. Anawahurumia na kutaka kuona kwamba wamelishwa. Lakini, mbinu yake ni kushirikiana na wanafunzi wake. Wana jukumu kuu role la kupata chakula, ambao unaongezwa, kisha kugawanya chakula hicho kwa watu.

Yesu anataka tutambue raslimali ambazo Mungu tayari ametupa na kuwapa wengine, hata ingawa zinaonekana kwamba si za maana, na kuzitumia ili kukimu mahitaji.

“Yesu anahitaji yale ambayo tunaweza kumletea. Huenda si mengi lakini anayahitaji. Pengine dunia imenyang'anywa miujiza baada ya miujiza na ushindi baada ya ushindi kwa sababu hatutaleta kwa Yesu tunacho na tulivyo. Ikiwa tungejiweka katika madhabahu ya utumishi wake, hatujui anachoweza kufanya pamoja nasi na kutupitia. Wakati mwingine tunasikitika au kuona haya kwamba hatuna zaidi ya kuleta – ifaavyo; lakini si sababu ya kukosa kuleta tunacho. Madogo daima ni makubwa mikononi mwa Kristo.”
-William Barclay

Tafakari:

Yesu anataka kushirikiana nasi vipi kwa ajili ya wengine? Anatuomba tuchukue hatua zipi maalum ili tuhakikishe kwamba mahitaji ya wanaotuzunguka yanatimizwa?

Kuhusu Mpango huu

A Biblical View On Social Change

Vikundi vingi vya Kikristo vinajishughulisha kukimu mahitaji ya kiroho ama ya kimwili. Tunafaa kuyapa yapi kipaumbele kama Wakristo? Tunaweza kujifunza nini kutokana na Biblia kuhusu mada huu?

More

Tungependa kushukuru Tearfund kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea:http://www.tearfund.org/yv