Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Mtazamo Wa Kibiblia Kuhusu Mabadiliko Katika JamiiMfano

A Biblical View On Social Change

SIKU 4 YA 5

Riziki


Unaweza kufikiri kuhusu wakati ambao ulihisi kwamba umelemewa na changamoto ama kazi fulani kwa sababu ilikuwa kubwa ajabu? Ulihisi vipi? Ulifanyaje?


Rafiki yangu, Mary, alihisi hivi. Maisha katika nchi ya Uganda yalikuwa magumu kwake. Mume wake alipotea, na kumwacha na watoto wadogo wanne. Aliishi katika nyumba iliyojengwa na udongo na kuezekwa nyasi na alikuwa na mbuzi mmoja. Mary alifanya kazi alipoweza na kupata mapato madogo, lakini hayakutosha na familia yake ilikuwa na njaa kila wakati. Naam, hakuna kilichobaki kulipa karo ya watoto wake.


Siku moja Mary alisikia kuhusu somo la Biblia liliotendeka katika kanisa mjini mwake. Alienda ingawa hata hakuwa muumini. Aliposikia kuhusu siku ambayo Yesu aliwalisha watu elfu tano, aligundua kwamba Mungu alijali watu wenye njaa! Somo liliangazia jinsi ambavyo Yesu aliwahimiza wanafunzi wake washirikiane ili kuhakikisha kwamba kila mtu alilishwa. Pamoja na wengine, Mary alishawishwa kuanza kupanga maisha tofauti sana ya badaaye na watoto wake.


Mary na familia yake wakaanza kupanda mimea ili kuuza na wakaweza kupata pesa ya kutosha kununua kuku wachache, kisha nguruwe, na hatimaye ng'ombe wawili. Maisha yao yalibadilika kabisa: lishe bora, mavazi, karo, nyumba bora, na dawa za kutibu ugonjwa.


Mary anang'aa siku ya leo. Anatembea kwa ukaribu na Bwana na ameona jinsi ambavyo Mola amemsaidia na kusaidia familia kupata riziki.


Tafakari:


Tunapofikiria kuhusu changamoto zinazokumba jammi zetu na ukosefu wetu wa raslimali, kuna himizo zipi maalum katika kisa hiki?


siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

A Biblical View On Social Change

Vikundi vingi vya Kikristo vinajishughulisha kukimu mahitaji ya kiroho ama ya kimwili. Tunafaa kuyapa yapi kipaumbele kama Wakristo? Tunaweza kujifunza nini kutokana na Biblia kuhusu mada huu?

Tungependa kushukuru Tearfund kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea:http://www.tearfund.org/yv

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha