Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Mtazamo Wa Kibiblia Kuhusu Mabadiliko Katika JamiiMfano

A Biblical View On Social Change

SIKU 3 YA 5

Kujitolea


Katika kifungu cha leo (Marko 6:35-36), tunapata wanafunzi wake katika nafasi ambayo inafanana na nafasi ambayo wengi wetu twajipata tunaposafiri na Yesu siku ya leo.


Madai yaliyotokana na kumfuata Yesu na kuwatumikia wengine yaliwachosha, na wanafunzi walitaka pumziko. Kisha, afueni yao mfupi ulikatizwa na mkusanyiko wa umati mkubwa ambao, bila shaka, ulikuwa na madai mengi.


Jioni ulipoanza wanafunzi wanalalamika kwamba umati hauonyeshi ishara za kuondoka hata ingawa pahali palikuwa patupu na hakuna chakula. Fikra yao ya kwanza ni kumwomba Yesu awaage, hakuna kitu kinaweza kutendeka.


Mara nyingi tunataka kufanya vivyo hivyo na wale ambao mahitaji yao yanashinda uwezo wetu kuyakimu. Tabia yetu ni kukaza mwelekeo wetu kulenga shida badala ya yanayowezekana. Vile vile, kama wanafunzi, tabia yetu ni kusukuma shida kwa Yesu atoe suluhu, badala ya kumwuliza namna ambavyo tunaweza kushirikiana. Sala zetu nyinginezo ni kama maombi ya wanafunzi—Yesu, ondoa jukumu hili kutoka daraja langu!


Tafakari:


Bila uaminifu wa Mungu, ingekuwa ngumu kwetu kupata riziki ya kila siku bila tumaini kwamba maisha yangebadilika. Lakini neno la Mungu limepandwa katika mioyo ya wote wanaoamini, na ametupa hamu ya kushirikiana ili kuona nguvu yake inayoleta mabadiliko.


Wanafunzi walikuwa na raslimali finyu lakini Yesu aliziongeza ili kulisha umati mkubwa. Je, una raslimali zipi ambazo pengine Mungu ataongeza na kutumia ili kubariki jamii yako? Pengine si mali, bali ustadi ama wakati.


siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

A Biblical View On Social Change

Vikundi vingi vya Kikristo vinajishughulisha kukimu mahitaji ya kiroho ama ya kimwili. Tunafaa kuyapa yapi kipaumbele kama Wakristo? Tunaweza kujifunza nini kutokana na Biblia kuhusu mada huu?

Tungependa kushukuru Tearfund kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea:http://www.tearfund.org/yv

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha