Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Mwanamume Wa KifalmeMfano

Mwanamume Wa Kifalme

SIKU 4 YA 5

Kuundwa Uwe Mkuu

Magari mengi ya kisasa yana udhibiti wa safari. Udhibiti wa mwendo ulivumbuliwa kama njia ya kudumisha kasi sawa iwe ya kupanda au kuteremka. Watu wengi hutumia udhibiti huo wanaposafiri mbali kama njia ya kuhakikisha wana mwendo usiobadilika. Hata hivyo, hutapata kipengele cha udhibiti wa usafiri kwenye magari ya mbio za magari. Kwa nini? Zimeundwa kwa ajili ya kasi, kuongeza kasi, utendaji na ukuu.

Shetani anataka kubembeleza mioyo ya wanaume ili kudhibiti mwendo na kuwafanya kuishi kwa kuridhika. Hataki uamke utambue kuwa Mungu amekuumba uwe mkuu. Mungu hakuwaumba wanaume wawe wastani, wasio na msukumo wala tamaa ya makuu u matamanio. Badala yake, aliwaumba wanaume wawe wakuu kwa ufalme wake.

Hebu tuangalie kwenye Mwanzo 12: 1 – 2. Kwenye aya ya 1, Mungu alimwita Abramu ili atii neno lake na kunyenyekea chini ya mamlaka yake. Kwenye aya ya 2 Mungu anaahidi ukuu unaofungamana na utii kwenye aya ya 1. Kwa maneno mengine, Abramu atakuwa na tajriba ya ukuu unaotajwa kwenye aya ya 2 ikiwa angetii amri iliyoko kwenye aya ya 1. Waona, unyenyekevu na ukuu unafungamana. Juu ya yote, kuna njia ya kuwa mkuu. Wanaume wengi sana wanataka kuwa wakuu lakini hawataki kutumia njia ya Mungu kufikia huko. Wanataka kufika huko kwa kujikweza wenyewe, wakitumia madaraka na vitisho. Katika uchumi wake Mungu, ukuu huja kwa utumishi si kwa kutawala. Ukuu wa kidunia hutokea tunapojaribu kujiinua wenyewe. Ukuu wa kweli hutokea wakati ustawi wa watu wengine ndio kitovu. Katika ufalme wa Mungu, Yeye hutafuta wanaume watakao tumika chini ya utawala wake kwa makusudi Yake. Na Mungu anapowapata watumishi, Yeye huwanyanyua. Anawakuza. Anawafanya kuwa wakuu.

Acha kujaribu kujiinua mwenyewe. Ukitaka kuwa mkuu, nyenyekea chini ya utawala wa Mungu, na anza kutumika. Ukifanya hivyo, utagundua kweli hii: kadri mtumishi alivyomkuu, ndivyo mtu anavyokuwa mkuu.

Kwa kuwa utumishi umefungamana na ukuu, ni katika njia zipi waweza kuwa mtumishi bora?

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Mwanamume Wa Kifalme

Katika historia yote, Mungu daima amewatafuta na kuwatumia wanaume kuendeleza ajenda ya Ufalme wake. Shetani anajua hili, ndiyo maana anataka kuwafungia na kuwahasi wanaume. Ulimwengu wetu unaendelea ukizorota kwa sababu...

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha