Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Mwanamume Wa KifalmeMfano

Mwanamume Wa Kifalme

SIKU 1 YA 5

Wako Wapi Wanaume?

Ukisikiliza kwa umakini unaweza kusikia kilio kwa wanaume halisi wajitokeze. Inaweza kusikika kutoka kwa kina mama walioachwa na sasa wanawalea watoto wao pekee yao. Inaweza kusikika kutoka kwa wakuu wa shule na waalimu wanaoongoza kwenye mstari wa mbele katika mifumo yetu ya elimu. Inaweza kusikika kutoka kwa maafisa wa polisi na majaji wakipigania kudumisha utaratibu. Inaweza kusikika kutoka kwa wachungaji wakati wa vikao vya ushauri. Inasikika kutoka kwa waajiri wanaotaka kudumisha uzalishaji mahala pa kazi. Je! Unaisikia?

Mpo wapi – nyie wanaume? Ni kama sanamu chukizo la mtu theluji. Kuna ushahidi pande zote. Nyayo.Kuonekana kifupi.Picha ya siri hapa na pale. Lakini mwanamume mwenyewe hapatikani popote.

Katika Ezekieli 22:30, Mungu asema, “Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, atakayelitengeneza boma, na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka, kwa ajili ya nchi, nisije nikaiharibu, lakini sikuona mtu. Ikiwa Mungu mwenyewe hangeliweza kumpata mwanamume halisi, basi ni vigumu kumpata mwanamume halisi.

Inaonekana kuwa hilo hilo ni kweli leo. Kuna watu wengi wa kiume na wavulana wengi wanaoweza kupatikana, lakini kunaupungufu wa wanaume. Hili laelekea kwa hitimisho kwamba, - kuna utofauti mkubwa sana kati ya kuwa mtu aliye wa kiume na kuwa mwanamume. Lakini hebu tuchukue hatua hiyo moja zaidi. Lakini bado kuna tofauti kubwa kati ya kuwa mtu mwanamume na kuwa mwanamume halisi – Wwanaume halisi, kulingana na ufafanuzi wa Mungu kuhusu uanaume wa kibiblia – ni wanaume wa Kifalme, wanaoelewa kwamba Mungu amewaumba wawe wakuu, watawale na kuwaboresha wale wote walio chini ya ushawishi wao. Wanaume wanapojifunza kutawala chini ya Mungu, tutamwona Mungu akitimiza mpango wake wa maisha yetu, na kwa kupitia maisha yetu, tutaadhiri familia zetu, makanisa na jumuiya

Ikiwa kuna tofauti kati ya kiume na mwanamume, unaweza kuelezea vipi uanaume?

Andiko

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Mwanamume Wa Kifalme

Katika historia yote, Mungu daima amewatafuta na kuwatumia wanaume kuendeleza ajenda ya Ufalme wake. Shetani anajua hili, ndiyo maana anataka kuwafungia na kuwahasi wanaume. Ulimwengu wetu unaendelea ukizorota kwa sababu...

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha