Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Mwanamume Wa KifalmeMfano

Mwanamume Wa Kifalme

SIKU 5 YA 5

Acha Kutoa Udhuru

Wakati timu zinapokuwa na misimu mbaya katika NFL, kocha mkuu anafukuzwa. Makocha hawarushi mpira unaokamatwa na timu pinzani. Hawachezi tafuti tafuti mpira. Hawaotei, au kukosa kunyanganya mpira. Lakini wanafukuzwa kazi. Sababu ya makocha kufukuzwa kazi japo hawafanyi makosa yoyote ni kwa kuwa wanawajibika kwa timu. Wanaweza kutoa visingizio vyote wanavyotaka. Wanaweza kunyoosha kidole na kupitisha lawama, lakini bado wao ndio wanawajibika.

Adamu na Hawa walipofanya dhambi, Mungu alikuja kumtafuta Adamu na kusema, “Uko wapi?” Hakuuliza, “Adamu na Hawa, mko wapi nyote?” Hiyo ni kwa sababu Mungu anawawajibisha wanaume. Ikiwa unataka kutawala, na ikiwa unataka kuwa mkuu, basi lazima uelewe kuwa unawajibika kwa kila kitu chini ya eneo lako la ushawishi. Hii inamaanisha kuwa huwezi kunyoosha kidole. Huwezi kupitisha lawama. Huwezi kuendelea kutoa visingizio.

Acha nikuambie kuhusu mtu mmoja mkuu katika Biblia. Pengine hujawahi kusikia habari zake hapo awali kwa sababu kuna aya mbili tu katika Maandiko kumhusu. Jina lake ni Shamgari, na aliokoa taifa zima la Israeli kutoka kwa Wafilisti. Hakuwa mwanajeshi wala mwanasiasa. Kuliko matarajio yaliyoko, alikuwa mkulima wa kawaida tu. Basi ni jinsi gani aliokoa Israeli? Hakusubiri kitu kitokee. Hakusubiri wengine wajiunge na pambano hilo. Hakungoja hadi apate silaha bora zaidi. Hakutoa udhuru wowote. Badala yake, aliona hitaji lililokuwepo na kulitimiza kwa rasilimali alizokuwa nazo.

Hivi sasa, baadhi yenu wanaume mnaweza kuwa mmekata tamaa. Huenda tayari umekosea. Labda ulifanya makosa na mke wako, watoto wako, kazi yako au na fedha zako. Haijaisha. Usikate tamaa. Acha kutoa udhuru. Fanya vyema ulipo sasa, na umruhusu Mungu ashughulikie mengine.

Tunatumahi kuwa mpango huu ulikuhimiza. Kwa habari zaidi kuhusu wizara, bofya hapa.

siku 4

Kuhusu Mpango huu

Mwanamume Wa Kifalme

Katika historia yote, Mungu daima amewatafuta na kuwatumia wanaume kuendeleza ajenda ya Ufalme wake. Shetani anajua hili, ndiyo maana anataka kuwafungia na kuwahasi wanaume. Ulimwengu wetu unaendelea ukizorota kwa sababu...

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha